BREAKING NEWS!!
Aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC 🇹🇿,Hassan Dilunga 'HD' ameanza mazoezi na Kikosi cha Simba chini ya Uangalizi maalumu kutoka Kwa Daktari wa Kikosi Cha Simba,Edwin Kagabo
Dilunga anarejea Simba baada ya kukaa Nje ya Uwanja Kwa zaidi ya Mwaka Mmoja akiuguza jeraha lake la goti na hatotumika Msimu huu kwakuwa jina lake halikusajiliwa kwenye Orodha ya Wachezaji wa Simba Msimu huu hivyo anaweza kusajiliwa na Simba kwenye Dirisha lijalo la Usajili baada kujua maendeleo ya afya yake.
