Wanachama zaidi 100 wa klabu ya Simba wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuuchunguza Uchaguzi mkuu wa klabu yao uliofanyika Januari 29, 2023.
Wanachama hao wamedai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na viashiria vya rushwa na uvunjifu mkubwa wa taratibu za uchaguzi.