Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Desemba 15, mabosi wa Simba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ pamoja na benchi la ufundi chini ya Kocha Juma Mgunda watafanya kikao kizito kuhusu hatma ya usajili, huku Cesar Manzoki akitarajiwa kutua nchini.
Mpango wa Simba kumpata straika wa Dalian Professional FC ya China, Manzoki huenda ukapotea kutokana na mkwanja anaopata mshambuliaji huyo.
Kabla ya kujiunga na Dalian, Manzoki alikuwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba uliyotakiwa kuanza mwanzo wa msimu huu ila ilikuwa ngumu kumpata kutokana na timu yake ya wakati huo, Vipers ya Uganda kudai bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi.
.jpeg)